Magonjwa ya Kuku
IIi uweze kudhibiti magonjwa ya kuku yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja.
Yapo magonjwa ambayo yanaweza kuangamiza kundi lote la kuku katika muda mfupi. Jihadhari na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo unaweza kuyazuia.
- Kuku kupoteza hamu ya kula.
- Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu (Kutochangamka).
- Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
- Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. – Macho kuwa na rangi nyekundu.
- Kujikunja shingo.
- Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na machoni.
- Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
- Kukonda.
- Kukohoa.
![]() |
| Kuku akichanjwa |
UGONJWA | CHANZO | DALILI | KINGA / CHANJO |
|---|---|---|---|
1. Kideri (NewCastle) | Virusi |
|
|
2. Kuhara damu (Coccidiosis) | Bakteria |
|
|
3. Ndui ya kuku (Fowl Pox) | Virusi |
|
|
4. Mafua ya kuku (Fowl Cryza) | Bakteria |
|
|
5. Kuharisha Nyeupe | Bakteria |
|
|
Njia kuu za ujumla za kudhibiti magonjwa ni:
- Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyevu
- Matandazo yakichafuka yabadilishwe.
- Vyombo vya maji visafishwe kila siku
- Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa kirahisi
- Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki salama
- Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo ya virusi
Hayo ndo magonjwa ya kuku kwa ufupi lakini tumeakuandalia makala zingine zinazohusiana na ufugaji wa kuku, hizi hapa chini, bofya kuzisoma:
Una tatizo kama hili shambani kwako?
Nikusaidie kutambua tatizo na kupunguza gharama. Ushauri kwa simu ni TSh 20,000 kwa kipindi, na ziara shambani ni TSh 100,000 + nauli.
Omba ushauri wa kulipia ↗Abdul Karim, Mtaalam wa Kilimo. Nina shahada ya Kilimo kutoka SUA na miaka 10 ya kilimo kwa vitendo. Makala hii ni bure, na ushauri wa kibinafsi ni huduma ya kulipia kupitia Mogriculture TZ.
